Mshambuliaji wa klabu ya Enugu Rangers ya nchini Nigeria, Ifeanyi George (26) amefariki dunia kwa ajali ya gari alipokuwa akirejea Jijini Lagos, baada ya ligi kuu ya soka nchini humo kusimamishwa kutokana na hatari ya Virusi vya Corona.
Nyota huyo wa Super Eagles, Ifeanyi George ameripotiwa kupata ajali leo siku ya Jumapili machi 22,2020 akiwa ndani ya gari na watu wawili ambao pia wameripotiwakufariki dunia.
Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa Enugu Rangers imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kukiri kuwa nyota wao Ifeanyi George akiwa na marafiki zake waili ndani ya gari hilo akiwemo mchezaji mmoja wa kikosi B wamefariki dunia.