HABARI

Mzee wa miaka 101 apona virusi vya Corona nchini Italia, Yaelezwa ilivyokuwa

Ripoti kutoka hospitali ya Jiji la Rimini Kaskazini mwa nchi ya Italia, inaeleza kuwa Babu mwenye umri wa miaka 101 ameruhusiwa kutoka Hospitali baada kupona ugonjwa wa virusi vya Corona.
Picha ya mzee huyo akipatiwa matibabu hospitalini
Mzee huyo ambaye amejulikana kwa jina la Mr P alizaliwa mwaka 1919, ameweka rekodi ya kuwa mtu mzee aliyeweza kushinda kupona ugonjwa huo baada ya kuaminika kuwa unaangamiza zaidi wazee.
Akitoa taarifa hiyo kiongozi wa hospitali  ya  Rimini Gloria Lisi, ameviambia vyombo vya ndani vya habari nchini humo kuwa  “Mr P ameruhusiwa kutoka hospitali siku ya Alhamisi jioni na kufuatwa na familia yake amekuwa mtu wa pili kupona ugonjwa huu,  na ametufundisha kuwa hata mtu mzee mwenye umri kama wake anaweza akapona, yajayo hayaandikwi“.
Aidha  amesema siku hiyo ya Alhamisi pekee amepokea kesi mpya za wagonjwa wa virusi vya Corona 1189, Pia shirika la Afya nchini humo limesema asilimia 86 ya vifo vilivyotokea kutokana na ugonjwa huo ni wazee walio na umri wa miaka 70 na kuendelea.

About the author

kidevu

Leave a Comment