HABARI

Meya wa Manispaa ya Iringa ‘CHADEMA’ Alex Kimbe, Ang’olewa madarakani baada ya kupigiwa kura za kutokuwa na imani nae

Meya wa Manispaa ya iringa, Alex Kimbe ameondolewa kwenye nafasi yake baada ya kupigiwa kura 14 za kutokuwa na imani na yeye kati ya Madiwani 28, kufuatia kutuhumiwa kuwa na matumizi mabaya ya ofisi yake.

Meya wa Manispaa ya iringa, Alex Kimbe
Kura hizo zimefanyika leo katika Manispaa y Iringa, ambapo katika kikao hicho Madiwani 14 walikuwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku Madiwani 12 wakitoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kwa mujibu wa Mwakilishi wa EATV mkoani Iringa Mwajuma Hassan ameeleza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Meya Alex Kimbe amesema bado anajitambua kuwa yeye ni Meya halali.

About the author

kidevu

Leave a Comment