HABARI

Madee “Mwana FA pole kwa Corona ukipona tunakukaribisha mtaani, Nikiwa kama Yanga natamani ligi ifutwe Simba wasiwe mabingwa”

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na C.E.O wa MMB Madee amefunguka mengi hasa kuhusu gonjwa linalotusumbua kwa sasa gonjwa la Corona.

Akiongea na Bongo5 Madee ametumia furasa hii kuwashauri watu kuweza kuchukua tahadhari dhidi ya gonjw ahili hatari kabisa la Corona ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu na unashauriwa kuwa kama huna kitu kinachokufanya uzunguke mitaani au kusafiri basi ni vyema ukatumia ndani kwako.
Mbali na hilo Madee amempa pole msanii mwenzake Mwan FA na kusema kuwa anaamini siku sio nyingi atakuwa tena mtaani na wana mkaribisha sana na kumuombea apone haraka.
Madee pia ameongelea kuhsuu ligi kuu nchini Tanzania na Uingereza na kusema kuwa simba wanastahili kabisa kuwa mabingwa licha ya watu wengi kusema ligi ifutwe. Madee ameongeza kuwa Simba wamefanya kila linalohitaji ili kuwa mabingwa na wamefanikiwa hivyo endapo ligi itafutwa watakuwa hawajatendewa haki licha ya yeye kuwa shabiki wa Yanga na ngetamani kuona ligi inafutwa lakini sio uungwana, “Ni kama Liverpool walivyopambana halafu leo uambiwe ligi inafutwa watakuwa wanaoenewa, Liverpool wanastahili kabisa ubingwa mwaka huu, na tunaomba ugonjwa huu uishe ili mipira iweze kurejea tena”

About the author

kidevu

Leave a Comment