HABARI

Watu milioni 3.3 wakosa ajira Marekani kutokana na virusi vya corona

Kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya corona nchini Marekani kumesababisha ongezeko kubwa la wanaosajiliwa kwenye orodha ya wasio na ajira, na kufika watu milioni 3.3, idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini humo.

Ripoti ya wasio na ajira ambayo ni utaratibu wa kawaida nchini Marekani, mara hii imekuwa mstari wa mbele katika mgogoro uliozuka baada kufungwa kwa migahawa, maduka, mahoteli na biashara nyingine.
Karibu kila jimbo la Marekani limeyataja maradhi ya COVID-19 kama sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi ya wasio na kazi, kunakokwenda sambamba na athari hasi katika sekta za chakula, hoteli, burudani, afya na usafiri.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wamekuwa wakitoa tahadhari juu ya madhara yatakayotokea katika sekta sekta ya ajira, lakini wengi walikuwa wakibashiri kiwango cha chini, cha watu takribani milioni 1.5.

About the author

kidevu

Leave a Comment