HABARI

Corona ni Ushahidi Kuwa Watumishi wa Afya Wanatakiwa Kulipwa Vizuri Kuliko Wengine

Mdau wa JamiiForums.com anasema hali ya #corona kwa nchi za Ulaya kwa sasa na hatari inayowakabili Watumishi wa sekta ya afya duniani ni ushahidi tosha kuwa kada hii ni kada muhimu na nyeti sana kuliko kada zingine zote

Anasema ni kweli karibu kila kada/kazi ina hatari zake, lakini kada ya afya ina hatari kubwa zaidi hasa yanapotokea majanga ya maradhi ya mlipuko kama ilivyo #Covid_19 kwa sasa
Sasa hivi watu tunaogopa hata kusogeleana huku tukiwa hatuna hata uhakika kuwa jirani zetu wana virusi lakini Madaktari na Manesi na Wafanyakazi wengine katika kada hii wao wanalazimika kuwahudumia wagonjwa licha ya hatari ya kupata maambukizi
Mbali na #corona, hata wanapohudumia wagonjwa wa magonjwa mengine, kama vile kuwafanyia upasuaj wagonjwa au kina mama wajawazito wenye magonjwa bado wanakuwa kwenye hatari kubwa tu ya wao kuambukizwa magonjwa hayo
Je, una maoni gani juu ya hoja ya Mdau?

About the author

kidevu

Leave a Comment