HABARI

Corona Tanzania, Naibu Waziri azungumza, agusia ufungaji mipaka “pombe haitibu corona, mask zinavaliwa na wagonjwa”

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Faustine Ndugulile amewataka Watanzania kupuuza uvumi wa kwamba unywaji pombe unasaidia kuua virusi vya corona huku akisema mask zinapaswa kuvaliwa na wagonjwa wenye corona badala ya kuvaliwa na kila mtu, amezungumzia pia kuhusu ishu ya kufunga mipaka ili kuzuia kuenea zaidi kwa corona.

“Pombe haizuii corona, maji tiririka na sabuni ni njia bora zaidi, matumizi ya sanitizer ni mbadala, wananchi wasipanic kwamba sanitizer zimepanda bei tunaweza kuzishusha kwamba kama wamepandisha sisi tunatumia maji, wanaosema sanitizer ni haramu ina pombe niwasihi tusianze kupotosha”  Ndugulile

About the author

kidevu

Leave a Comment