HABARI

Ni kwanini Trump amekua makini na matumizi ya dawa ya malaria kutibu coronavirus?

President Trump

Rais wa Marekani Trump anadai dawa inayotumiwa dhidi ya malaria imeithinishwa nchini Marekani kutibu coronavirus mpya.
Chloroquine ni moja ya madawa ya zamani sana yanayofahamika sana kutibu ugonjwa wa malaria.
Kwahivyo je rais ni sahihi na ni kipi kinafahamika juu ufanisi wake wa kimatibabu?
Chloroquine imekuepo kwa miongo kadhaa. Haitolewi tena katika mataifa mengi ya Afrika kwasababu ya kinga iliyojengwa na wadudu wa malaria.
Baadhi ya nchi zimetoa sheria ya kukabiliana na matumizi ya dawa hiyo, lakini imebakia kuwa maarufu miongoni mwa wale wenye sekta binafsi ya soko la madawa na inauzwa kwa kiwango kikubwa.
Hii ni dhahiri hasa nchini Nigeria ambako kumekua na ripoti za chloroquine kununuliwa sana katika maduka ya dawa na hivyo kusababisha upungufu, na kwa sehemu kubwa upungufu huo umechochewa na kauli ya Bwana Trump.
Kirusi cha corona
Image captionUtafiti unaendelea kuangalia ikiwa chloroquine inaweza kutibu Covid-19
Chloroquine bado haijaidhinishwa kwa tiba ya coronavirus
Rais Trump, katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari, alidai kwamba chloroquine imeidhinishwa kwa kwa ajili ya kutumiwa kwa matibabu ya coronavirus na Taasisi ya Marekani ya masuala ya Chakula na Dawa (FDA). Taasisi hiyo inahusika na utoaji wa vibali vya dawa nchini Marekani.
“Tutaweza kuwezesha upatikanaji wa dawa hiyo mara moja. Na hapo ndio FDA imekua bora. Wamepitia mchakato wa kuiidhinisha – imeidhinishwa.”
Kusema wazi, chloroquine imeidhinishwa kutibu magonjwa ya malaria ugonjwa wa viungo (arthritis). Hatahivyo, FDA imeweka wazi dawa hiyo haitibu watu Covid-19 coronavirus.
” Hakuna idhini ya FDA- ya matumizi ya dawa hiyo kutibu au kuzuwia Covid-19.”
Hatahivyo, FDA inasema kuwa utafiti unaendelea kuangalia ikiwa chloroquine inaweza kutibu Covid-19. Imesema pia kwamba imeagizwa na Bwana Trump kuanzisha kliniki ya majaribio ya kimatibabu ili kuichunguza dawa hiyo.
A female scientist in a coronavirus testing labHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanasayansi wa Marekani swameanza majaribio kuona ikiwa dawa ya chloroquine itasaidia kutibu coronavirus
Vipi kuhusu hali ya utafidi wa dunia juu ya coronavirus?
Haishangazi kwamba chloroquine imekua ni sehemu ya utafiti wa kuwasaidia wagonjwa wa coronavirus
Inafahamika sana, na ni nafuu na rahisi kutengeneza. Katika kuwatibu wagonjwa wa Malaria, dawa hiyo imekua ikitumika kupunguza joto la mwili na vidonda.
“Chloroquine ilionekana kuzuwia coronavirus katika tafiti za maabara. Kuna ushahidi kiasi kutoka kwa madaktari wakisema kuwa imeonekana kusaidia ” anasema James Gallagher, Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya.
Lakini la muhimuni kwamba hakuna ushahidi kamili wa majaribio ya tiba ambao umekamilika ambayo ni muhimu kuonyesha jinsi dawa inavyofanya kazi katika mgonjwa halisi, ingawa yanafanyika katika mataifa ya Uchina, Marekani, Uhispani na Uingereza.
Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, linasema Shirika la Afya Duniani (WHO)
Image captionMchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, linasema Shirika la Afya Duniani (WHO)
Shirika la Afya Duniani linasema kuwa hadi sasa hakuna ushahidi wa ufanisi wake, lakini dawa hiyo ni sehemu ya majaribio yanayoendelea
” Ili kufahamu ni dawa gani inaweza kufanya kazi katika kutibu maambukizi ya virusi tunahitaji kufanya majaribio ya kimatibabu ili kupata ushahidi kamili kujua ikiwa inafanya kazi au la ,”anasema Profesa Trudie Lang, mkurugenzi wa mtandao wa Afya ya dunia katika Chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza.
Watu wengi tayari wameanza kutaka kuifahamu zaidi dawa hasa katika mtandao.
Idadi ya watu wanaotafuta maelezo yake imepanda katika kipindi cha wiki iliyopita, kwamujibu wa data za Google za taarifa zinazosakwa zaidi – Google Trends d, na entrepreneur Elon Musk alisababisha gumzo pale alipotuma ujumbe wa twitter uliokua na taarifa alizozisaka kuhusu dawa hiyo.

Unaweza pia kusoma:

Taarifa zidi za coronavirus

Ununuzi wa hofu nchini Nigeria

Janga la coronavirus linazungumziwa na karibu kila mtu nchini Nigeria katika makanisa, misikiti, na shule anasema Daniel Semeniworima, mwandishi wa BBC idhaa ya Pidgin mjini Lagos.Nyingi kati ya nyumba nchini Nigeria bado zinatumia dawa ya chloroquine kwa matibabu ya malaria ingawa ilipigwa marufuku mwaka 2005.
Taarifa ya juu ya utafiti wa mwezi Februari nchini Uchina juu ya matumizi ya chloroquine kwa coronavirus tayari yameibua mjadala mkubwa mjini Lagos, kwa hiyo watu wananunua na kuiweka dawa hiyo.
Kufuatia kauli ya Bwana Trump kuhusu chloroquine kama tiba ya coronavirus treatment, maduka ya kawaida na yale ya madawa yaliuza haraka na kumaliza kabisa dawa hiyo
Lakini kituo cha udhibiti wa magonjwa nchini Nigeria kimewaambia watu waache kuitumia.
” WHO BADO haijaidhinisha matumizi ya chloroquine kwa ajili ya tiba ya #COVID19.”
Daniel Semeniworima anasema kuwa watu wanachukua maamuzi ambayo hayana maelezo kubaki salama lakini hili linakua na athari mbaya za kimatibabu.
Imeripotiwa kwamba sasa Lagos inakabiliana na tatizo la watu ambao wameathiriwa kwa kumeza chloroquine zaidi ya dozi ya kawaida.
Jinsi nchi za Africa zinavyodhibiti coronavirus

About the author

kidevu

Leave a Comment