HABARI

Djourou na Alex Song waachwa kisa kugoma kukatwa mshahara sababu ya corona

Club ya Sion ya Uswiss imewaacha wachezaji wake 9 waliokataa kukatwa mshahara wakati huu Ligi yao ikiwa imesimama kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona.
Mastaa wa zamani wa Arsenal Alex Song na Johan Djourou ni miongoni mwa wachezaji wa club hiyo walioachwa kwa sababu ya kugoma kukatwa mishahara yao.
Sion kwa mujibu wa SDA News na RSI TV wamewaacha nahodha Xavier Kouassi, Pajtim Kasami, Ermir Lenjani, Seydou Doumbia, Mickael Facchinetti, Christian Zock na Birama Ndoye kwa sababu ya club hiyo ilitaka kuwakata mshahara kwa sababu hawachezi Ligi kwa sasa.

About the author

kidevu

Leave a Comment