Taarifa za kifo chake zilitangazwa na mwanae Binti Liza Monet ambaye pia ni mwanamuziki , aliandika kwenye kurasa yake ya twitter .
” Baba yangu amefariki kutokana na virusi vya korona majira ya asubuhi… Asante kwa kuheshimu kumbukumbu yake.
Yeye ni historia kubwa ya muziki wa Sukouss au maarufu kama bolingo ambayo watu wa Kongo wameupoteza . Moyo wangu umeumia sana na sina nguvu maana , Baba yangu ambaye nilimpenda sana ameondoka”
Aurlus Mabelé amefariki akiwa na umri wa miaka 67, mwanamziki huyu wa DRC ambae muziki wake ulikuwa maarufu sana mnamo 1990.
Wakati kifo kimempata tayari alikuwa na ugonjwa wa koo kuvimba kwa takribani miaka kumi hivi.
Hali yake hiyo ya udhaifu ya tangu zamani haikumruhusu kukabiliana na jango hilo ambalo limesabisha maelfu ya maafa duniani.
Mnamo mwaka 2005, Aurlus Mabelé aliugua maradhi ya akili .
Arlus mabele alianzisha bendi ijulikanayo kama loketo mnamo mwaka 1986, iliweza kujipatia umaarufu Afrika mzima haswa muziki wake wakuchangamsha maarufu kama soukous.
Bendi yake iitwayo ‘loketo’ maana yake ni mauno.
Vilevile mpaka anakufa ni zaidi ya albamu zake milioni 10 zilizouzwa ulimwenguni katika zaidi ya miaka 30 ya tasnia yake ya muziki.
Mashabiki wake walimwita mfalme wa soukous-Kifo chake kimezua taharuki katika maeneo mengi ya Afrika.
Huku wengine wakihakikisha kuwa ugonjwa wa corona unauwa watu weusi pia.
Baada ya msanii Aurlus Mabele kufariki kwa Corona Ufaransa, Utata waibuka kuhusu kuzikwa Congo au Ufaransa
Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wametuma salamu zao za rambirambi kwa familia, marafiki na mashabiki wa mwanamuziki huyo.
Mabélé, ambaye jina lake asili ni Aurélien Miatsonama, alitokea Congo-Brazzaville na kuhamia Ufaransa mwaka 1980.
Mazungumzo na serikali ya Congo bado yanaendelea ili mwanamuziki huyo arudishe kuzikwa nyumbani.
Lakini kwa sasa mwili wake hauwezi kusafirishwa kurejea Congo mpaka katazo la kusafiri liondolewe.
Ikumbukwe kuwa Mabélé aliufanya muziki wa soukous ujulikane ulimwenguni kote.
Chini ya jina lake asili Aurélien Miatshonama, Mabélé alirikodi mimbo mingi ambayo ilipendwa katika bara zima la Afrika tangu miaka ya 1970s kama vile wimbo wa Embargo, Zebola na Waka Waka.
Baadae alihamia Ufaransa na kuunda bendi ya Loketo, nyimbo zake nyingi alitumia lugha ya Lingala ambayo inatumika DR Congo na Congo-Brazzaville.