Waziri wa Afya nchini Rwanda Anastase Shyaka alitangaza hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na coronavirus
Wizara ya afya nchini Rwanda imetangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.
Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.
Walipatikana na maambukiz hayo wote walikua wametoka katika nchi za ng’ambo hivi karibuni.
Wizara ya afya imewataja watu hao sita kuwa ni:
- Mwanamke Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 na mtoto wake wa miezi 10. Mume wake mama huyu alikuwa pia amepatikana na virusi siku zilizopita.
- Mtoto wa miezi 10 ndiye mtu mwenye umri mdogo zaidi aliyewahi kupatika ana coronavirus nchini Rwanda tangu ilipogundulika nchini humo wiki iliyopita
- Mwingine ni Myanrwanda mwenye umri wa miaka 32 aliyefika nchini Rwanda akitokea wageze mu Dubai tarehe 19/03/2020
- Mwanaume kutoka Sweden waliyefika Rwanda 03/03/2020 lakini akaonyesha dalili za coronavirus tarehe 18/03/2020
- Mwanaume Myarwanda mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekua akifanya safari katika mataifa ya kigeni ambaye alipatikana na dalili tarehe 18/03/2020
- Na mwingine ni Mwanaume Mnyarwanda mwenye umri wa maika 24 aliyefika Rwanda tarehe 19/03/2020 kutoka India kupitia Doha – Qatar.
Kulingana na wizara ya afya nchini humo wagonjwa wpote wametengwa na wanaendelea kupata matibabu.
Inawaomba watu wote waliofika nchini Rwanda katika kipindi cha siku 14 zilizopita kujitenga binafsi kwa siku 14 na kufuata maagizo yaliyotolewa juu ya coronavirus.
Hatua zilizochukuliwa na Rwanda kudhibiti coronavirus
Waziri wa Afya nchini humo Anastase Shyaka alitangaza kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.
Matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini vimeahirishwa na wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.
Shirikisho la Sola la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.
Maeneo ya umma na maeneo yote ya utoaji wa huduma yameagizwa kuweka vitakasa mikono kwa ajili ya umma unaotembelea maeneo hayo.
Raia wamehimizwa kukaa nyumbani na kuepuka matembezi yasiyo ya maaana na kunawa mikono mara kwa mara kwa muda wa sekunde 20.
Hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.
Baadhi ya dalili za coronavirus ni kikohozi, kushindwa kupumua vema na uchovu.