Kama unasimuliwa na mtu unaweza kusemani uzushi lakini ukweli ni kwamba Msanii wa Bongo Fleva Wema Sepetu anamiliki mbwa ambaye anamuita kuwa ni mtoto wake na umbwa huyo ana akaunti ya Insagram.
Wema ambaye ni maarufu sana kwa katika tasinia ya muvi za bongo katika mtandao huo wa instagram ana wafuasi milioni 6.7 na mtoto (Mbwa) wake ana wafuasi takribani 3,000.
Tofauti na mbwa mwingine Mbwa wa wema ambaye anaitwa Vanillanunu anaposti na kuandika maelezo ya posti zake na mama yake humlalamikia na kumuonya pale anapokosea kama juzi alipochezea nguo za mama yake na kuzichana.
Ishu sio wema na watoto wake katika mitandao mjadala ulioibuka ni mbwa huyo kuwa na akaunti ya Instagramu tena yenye wafuasi wengi kuliko hata wengi wetu nikiwemo mimi.
Wengine waliohoji majukumu ya mtoto huyo mpendwa wa Wema na wengine wanamsfia kuwa ni mzurii.