Binti mmoja mkazi wa Kiteto mkoani Manyara amesimulia tukio lake la kuozwa kwa mwanaume kwa mahari ya shilingi elfu kumi.
Binti huyo aliolewa mwaka jana akiwa na miaka kumi na mwanaume mwenye miaka 48 ajulikanaye kwa jina la Baraka Meleu ambaye alitoa elfu kumi tu kwa wazazi wake na kukabidhiwa.
Binti huyo anadai kuwa alikuwa akiteswa na mwanaume huyo baada ya kumuoa ikiwa ni pamoja na kumlazimisha kufanya tendo la ndoa kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali kwenye kidonda kilichotokana na kukeketwa ambacho kilikuwa bado hakijapona.
Binti huyo alilazimika kuomba msaada kwa mama mmoja aliyekuwa jirani yao na alifanikiwa kumtorosha na kwenda kituo cha polisi ambapo pia walipeleka malalamiko kwenye ofisi za maendeleo ya jamii.
Mwanaume ambaye amemuoa binti huyo amepatikana lakini wazazi wa binti wanadaiwa kutoroka na bado haijajulikana walipo