Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kutomtenga wala kumnyanyapaa Isabella kwa kuwa kwa sasa hali yake ya kiafya imeimarika na yuko tayari kwa ajili ya kurejea nyumbani.
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Machi 26, 2020, wakati akitoa taarifa kwa umma, kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini na kwamba hadi sasa Tanzania ina jumla ya wagonjwa 13 na tayari wasafiri zaidi ya Milioni 1 wamekwishafanyiwa vipimo vya joto la mwili.
“Kuanzia Januari hadi sasa jumla ya wasafiri Milioni 1.8 wamefanyiwa ukaguzi kwa kupimwa joto la mwili, hadi sasa hatuna maambukizi ya ndani na Mgonjwa wetu wa kwanza Isabella amepona, tumempima sampuli mara tatu na imeonesha Negative, tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani, jamii imkubali, impokee bila kumnyoshea vidole, bila kudhalilishwa, bila kutukanwa wala kudharauliwa” amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa mgonjwa wa 13 alipatikana mkoani Kagera na ni dereva wa magari makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga na shughuli zake anafanyia kati ya Burundi, DRC na Tanzania.
duuh sio mchezo