HABARI

Ndege ya kijeshi ya Urusi yaanguka katika Bahari Nyeusi

Shirika la habari la Urusi limeripoti kuwa ndege ya jeshi la nchi hiyo chapa SU-27 ilianguka katika Bahari Nyeusi jana usiku, na kwamba operesheni imeendelea hadi leo asubuhi kumtafuta rubani wa ndege hiyo.

Shirika hilo limesema ndege hiyo ilipotea kwenye rada ikiwa umbali wa kilometa 50 kutoka mji wa Feodosia katika rasi ya Crimea, ambayo Urusi imeinyakua kutoka Ukraine.
 Wafanyakazi wa uokozi wanasema wamefuata ishara za njia ya mawasialiano ya dharura ya redio, ambayo imesikika mahala ambapo pameelezwa kuwa mbali sana na walipoanzia uchunguzi wao, hii ikiwa ni kwa mujibu wa afisa wa serikali aliyenukuliwa na shirika la habari la Tass.
Imearifiwa kuwa ndege hiyo iliyoanguka ilikuwa katika ujumbe ambao hata hivyo maelezo yake zaidi hayakutolewa. Shughuli hizo za uokozi znatatizwa na hali mbaya ya hewa.

About the author

kidevu

Leave a Comment