HABARI

TIGER WOODS APATA AJALI

 
 MCHEZAJI maarufu wa Golf, Tiger Woods, amepata ajali baada ya gari lake kupinduka wakati akiendesha mwenyewe nje kidogo ya jiji LA Los Angeles.

 

Woods amejeruhiwa miguu yake yote miwili na hawezi kusimama peke yake. Tayari amewahishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu ambapo amefanyiwa upasuaji tayari.

  

Mshindi huyo mara 15 wa mchezo wa gofu, mwenye miaka 45 alitolewa kwenye eneo la ajali na wahudumu wa zima moto na wahudumu wa afya. 


Mkuu wa Polisi, Alex Villanueva, baadaye alisema kuwa Woods alikuwa hai na mwenye fahamu katika eneo la ajali.


 Kisha alipelekwa hospitalini kwa gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha UCLA huko West Carson, California. 



Wakala wa Woods, Mark Steiberg alithibitisha kuwa alikuwa alifanyiwa upasuaji siku ya Jumanne na kutoa taarifa kuhusu majeraha yake

Katika mkutano na wanahabari , mkuu wa idara ya zimamoto ya kaunti ya LA Darlyl Osby alisema kuwa Woods aliondolewa kwenye gari aina ya GV80 luxury SUV kwa kutumia shoka. 


Aliongeza: ”Ninaelewa kuwa ni majeraha mabaya kwa miguu yake yote. Hakukuwa na majeraha mengine yaliyohatarisha maisha yake ninavyofahamu.”

About the author

kidevu

Leave a Comment