DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa jana Febrari 23 walistahili kushinda kwa kuwa walijipanga vizuri jambo ambalo limewapa matokeo chanya.
Wakiwa Uwanja wa Mkapa mashabiki wa Simba wainyanyuka kwenye viti dakika ya 30 kushangilia bao lililopachikwa na Luis Miquissone kwa shuti kali akiwa nje ya 18.
Bao hilo alifunga kwa pasi ya kiungo Clatous Chama iliwafanya Al Ahly wasiamini wanachokiona kwa kuwa Simba waliweza kulinda bao hilo kwa muda wa dakika 60.
Ushindi huo unaifanya Simba kuwa nafasi ya kwanza kwenye kundi A ikiwa na pointi 6 inafuatiwa na Vita Club ambayo jana ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Merreikh ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa haina pointi.
Al Ahly ipo nafasi ya tatu ikiwa sawa pointi na AS Vita wakiwa tofauti kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungana ndani ya uwanja.
Gomes amesema:”Tulistahili kushinda kwa kuwa wachezaji walikuwa tayari na walionyesha hilo ndani ya uwanja. Kwa namna yoyote ile wanastahili pongezi na kazi bado inaendelea,” .