HABARI

TANZANIA PRISONS: AZAM INABIDI WASHUKURU KWA KUPATA SARE

 

SHABAN Kazumba, kocha msaidizi wa Klabu ya Tanzania Prisons amesema kuwa wapinzani wao Azam FC inawabidi washukuru kwa sare waliyoipata Uwanja wa Azam Complex.

Ikiwa ugenini, juzi ililazimisha sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Kazumba amesema kuwa walijipanga kushinda mbele ya Azam FC jambo ambalo walilifanya kwa muda wote ndani ya uwanja ila walikosa bahati ya kufunga.

“Azam FC inawapasa washukuru kwa sare ambayo wamepata kwani tulikubaliana kwamba lazima tuwafunge pamoja na wachezaji wao wakubwa maana ukiangalia kikosi chetu wachezaji ni Polisi na raia sasa wana bahati wamepona.

“Kwa sare ambayo tumeipata kiufundi ninawapongeza wachezaji kwa kuwa inamaanisha kwamba uwezo wote ni sawa lakini bado hatujatimiza lile lengo la kuwafunga bado wanapaswa kushukuru,” amesema.

Ikiwa imecheza mechi 20 ipo nafasi ya 8 na pointi zake ni 26 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake ni 37.

About the author

kidevu

Leave a Comment