HABARI

KOCHA YANGA AJA NA MBINU MPYA ZA USHINDI

 


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa mechi zilizobaki utatumia mbinu mpya zitakazowafanya waweze kushinda ndani ya uwanja na kupata pointi tatu katika mechi zao za mzunguko wa pili.

Ikiwa inaongoza Ligi Kuu Bara baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na kujikusanyia pointi 49 ilianza kwa kusuasua mzunguko wa pili kwa kupata sare mbili mfululizo.

Ilianza mbele ya Mbeya City 1-1 Yanga, ngoma ilichezwa Uwanja wa Sokoine kisha mbele ya Kagera Sugar ubao ulisoma 3-3 ilikuwa Uwanja wa Mkapa na iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa mbinu anayokuja nayo kwa sasa ni kuwataka wachezaji wake wacheze kwa kujiamini na kutumia nafasi ambazo wanazipata.

“Wachezaji wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya uwanja ila walikuwa wakikosa kujiamini pale wanapoanza jambo ambalo linafanya matokeo kuwa magumu kupatikana.

“Kwa sasa nimewaambia kwamba wana kazi ya kufanya kwenye mechi zetu zote ambapo wanapaswa kujiamini na kutumia nafasi ambazo wanazipata.

“Naona kama wanakuwa wanashindwa kuzitumia nafasi kwa kuwa kwenye mechi zetu imekuwa hivyo hasa kipindi cha kwanza lakini haina maana kwamba hatuchezi,”.

About the author

kidevu

Leave a Comment