HABARI

IHEFU YAGOMA KUSHUKA DARAJA MSIMU UJAO

 

 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC amesema kuwa wana imani ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.

kwenye msimamo, Ihefu FC ipo nafasi ya 16 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na imekusanya jumla ya pointi 20.

Safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 13 huku ile ya ulinzi ikiwa imeokota nyavuni jumla ya mabao 28.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa vijana wake wana morali kubwa na kila siku anaona maendeleo kwao jambo ambalo anaamini litawapa nafasi ya kupata matokeo chanya.

“Bado kikosi kipo imara taratibu tofauti na awali kwa kuwa morali imekuwa kubwa na kuna wachezaji wenye uzoefu ambao wanawapa nguvu vijana ndani ya uwanja.

“Imani yetu ni kwamba tutakuwa ndani ya ligi msimu ujao hatuna mpango wa kushuka, hilo lipo wazi kwa sasa hesabu zetu ni kupata pointi tatu kwenye mechi zetu ambazo tunacheza,” .

Miongoni mwa wachezaji ambao wameongezwa na Ihefu chini ya Katwila ambaye alibwaga manyanga ndani ya Mtibwa Sugar ni Deogratius Munish,’Dida’, Andrew Simchimba, Rafael Daud na Oscar Masai. 

About the author

kidevu

Leave a Comment