HABARI

Wakazi wa jimbo la California, Marekani waamuriwa kubaki majumbani kudhibiti Virusi vya Corona

Jimbo maarufu zaidi nchini Marekani, California limewaamuru wakazi wake kukaa nyumbani ikiwa ni katika harakati za kujaribu kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.
Image result for San Francisco
Gavana, Gavin Newsom aliwaambia wakazi wa California kuwa watalazimika kutoka majumbani mwao pale tu kutakapokuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.
Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.
Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi.
Kwa ujumla wagonjwa karibu 250,000 kote duniani wamepatikana na virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa kupumua na takriban 9,900 wamekufa.
Amri ya California inamaanisha niniCalifornia Street, usually filled with cable cars, is seen empty in San Francisco, CaliforniaMitaa ya jiji la San Francisco jimboni California ambayo kwa kawaida hufurika magari kwa sasa ni mitupu
Gavana Newsom alisema hayo siku ya Alhamis jioni: “Wakati huu tunahitaji kuchukua maamuzi magumu. Tunahitaji kutambua hali halisi.”
Amri yake itawaruhusu wakazi kuondoka majumbani mwao kununua mahitaji ya nyumbani au dawa, au pale wanapotembeza mbwa au wanapofanya mazoezi ya mwili, lakini itawataka kuacha mikusanyika ya watu.
Itawalazimu biashara ambazo zinaonekana si za lazima kufungwa, huku ikiwaruusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.
Takriban nusu ya wakazi wa jimbo hilo wamekwishaanza kutekeleza hatua hizo kali, likiwemo Jiji la San Francisco.
Gavana Newsom ambaye anatoka chama cha Democratic amesema kuwa sehemu za jimbo hilo zimeshuhudia kuongezeka kwa viwango vya maambuzi ya coronavirus mara dufu kwa kila baada ya siku nne.
Alielezea hayo katika barua yake kwa rais Donald Trump siku ya Jumatano, akitoa wito wa msaada wa haraka kutoka kwa Serikali ya kuu.
“Tunatazamia takriban asilimia 56 ya watu- milioni 25.5 wataathiriwa na virusi vya corona katika kipindi cha wiki nane zijazo ,” Gavana Newsom aliandika.
Hadi sasa California imerekodi visa vilivyo chini kidogo ya 1,000 vya virusi vya corona na vifo 19, kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times.
Maeneo mengine yenye ”idadi kubwa” ya coronavirus ni yapi?
Kando na Jiji la New York na Washington, California ni miongoni mwa majimbo yaliyozongwa na janga la coronavirus.
Alhamisi pekee, rekodi ya maambukizi ya Covid-19 katika Jiji la New York ilionyesha kuongezeka mara dufu na kufikia hadi watu 3,954 – ikiwa ni kubwa kuliko watu idadi ya wagonjwa wa coronavirus katika nchi nzima ya Uingereza.
Meya Bill de Blasio aliiambia CNN kuwa jimbo hilo maarufu nchini Marekani litakosa vifaa vya kimatibabu katika kipindi cha wiki tatu ikiwa ”mlipuko” wa maambukizi utaendeela kwa kiwango cha aina hiyo.
Aliitaka serikali ya shirikisho kuisaidi New York kupata vifaa vya kusaidia kupumua 15,000, barakoa za upasuaji milioni 50 , na magauni ya 45 million, na vifaa vya madaktari vya kujikinga.
Meya alisema kuwa virusi vimewaua watu 26 katika jiji hilo..
Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Marekani Alhamisi iliwataka Wamarekani kuacha safari za nje ya nchi.

About the author

kidevu

Leave a Comment