HABARI

Wachezaji wa FC Barcelona wagoma makato ya 70% ya mishahara yao

Wachezaji wa FC Barcelona wapo katika mvutano mkubwa ndani kwa ndani na bodi ya timu yao kufuatia pendekezo la bodi hiyo la kutaka kuwakata mishahara.
Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu anaingia katika mvutano mzito na wachezaji hao kutokana club inataka kuwakata wachezaji hao kila mmoja asilimia 70 ya mshahara wake wakati huu Ligi ikiwa imesimama kwa sababu ya virusi vya corona.
Bodi ya wakurugenzi inapanga kufanya kikao kupitia video conference leo kujadili kuhusiana na makato hayo ya mishahara lakini kwa mujibu wa Diario Sport wachezaji hawajakubali makato ya asilimia 70.
Hadi sasa Hispania inaripotiwa kuwa takribani jumla ya watu 4000 wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa virusi vya corona na club za soka zinakata mishahara ya wachezaji ili kupunguza hasara.

About the author

kidevu

Leave a Comment