HABARI

Golikipa Italia apinga kukatwa mshahara “Sisi sio kama Ronaldo”

Golikipa wa Ligi daraja la kwanza Italia (Serie B) Alberto Paleari (27) ameeleza hisia zake kuhusiana na kinachoendelea na kusema kuwa sio kila mchezaji Italia na uwezo wa kipesa kama Cristiano Ronaldo.
Alberto ameyasema hayo kufuatia kutakiwa wachezaji Italia kukatwa mishahara yao katika kipindi hiki Ligi zikiwa zimesimama na wengine kushauriwa kuchangia katika mapambano ya virusi vya corona.
”Sisi sio kama Ronaldo kama tukikatwa mishahara yetu mwenye nyumba atakuja kupiga hodi (kudai kodi), kama watakata mshahara wake (Ronaldo) wa miezi miwili bado hatokuwa na tatizo la kifedha”
”Kama ingekuwa ni suala la kucheleweshewa mshahara kwa miezi miwili lakini baadae utapokea mishahara yote ya miezi miwili, mimi ningekubali bila hata kusita”
Kipa Alberto anayecheza Cittadella amesema hawezi kukubali kukatwa mishahara kwa sababu vipato vya ni vidogo na hawana pesa kama staa wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye yuko tayari hata kukatwa mshahara ili asaidie sio tu kwa sababi club inayumba kiuchumi.

About the author

kidevu

Leave a Comment