HABARI

Staa wa Rugby aliyejitolea kuwa dereva wa ambulance Italia

Staa wa mchezo wa Rugby nchini Italia Maxime Mbanda ,27, anayeichezea Zebre amejitolea kuwa dereva wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) nchini Italia wakati huu wa janga la corona.
Mbanda anafanya kazi saa 13 kwa siku bure, Italia inaonekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika wa virusi vya corona kiasi cha Cuba kuwapa madaktari zaidi ya 50 waongeze nguvu.
Maxime Mbanda ameelekeza nguvu zake katika kusaidia taifa lake wakati huu ambao Italia imesimamisha michezo yote ikiwemo Rugby kama njia ya kuondoa mikusanyiko inayoweza kusababisha maambukizi.

About the author

kidevu

Leave a Comment