HABARI

Staa wa Real Madrid kuadhibiwa kwa kukiuka sheria za karantini

Baba mzazi wa mshambuliaji wa Real Madrid Luka Jovic ameonesha kutokuwa na tatizo endapo mtoto wake Jovic ataenda jela kwa kosa linalodaiwa kuwa la kizembe la kupuuzia agizo la kukaa karantini Hispania.
Baada ya kusimama kwa Ligi Kuu Hispania LaLiga kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona, Real Madrid na wachezaji wengine walishauriwa kujitenga kwa siku 14 ili kubaini kama wako salama au la.
Jovic ambaye ni raia wa Serbia alikaa kwa siku chache na kabla ya muda kuisha aliamua kuondoka zake na kwenda nchini kwao Serbia akiwa anatokea Hispania nchi ambayo ina waathirika wengi wa corona kuliko Serbia, kitu ambacho kimemkwaza Rais wa Serbia.
Baba mzazi wa mchezaji huyo amekiri kuwa mwanae ambaye anachunguzwa kwa sasa anastahili adhabu, Jovic alipima corona akiwa Hispania na kukutwa negative na hakupaswa kusafiri hadi siku 14 ila amesafiri kurudi kwao Serbia na kuonekana sehemu za starehe na mpenzi wake.

About the author

kidevu

Leave a Comment