HABARI

Staa wa Chelsea amethibitika kupona corona

Staa wa Chelsea Callum Hudson-Odoi apona corona na kurejea katika maisha yake ya kawaida baada ya kutengwa wiki kadhaa nyuma Kwa kugundulika kuwa na maambukizi.
Odoi alikuwa staa wa kwanza wa soka England kugundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya corona, kwa sasa Odoi ameanza kufanya mazoezi binafsi baada ya kupona na kuendelea  na mfumo wa maisha yake ya kawaida.
Odoi alijitangaza kupata maambukizi hayo lakini alieleza kuwa anafuata taratibu za wataalam wa afya kama zinavyotaka, Ligi Kuu England ikiwa imesimama hadi April 30 2020 Odoi anaendelea na mazoezi binafsi ya kujiweka fiti akiwa nyumbani kwake.

About the author

kidevu

Leave a Comment