Uncategorized

Nilipewa Hirizi Nikaimeza, Nilitaka Nikitongoza Wanawake Nisikataliwe. Hali imekuwa Mbaya Sasa, Dada Yangu wa Damu Ananitaka Sasa

Natumaini mko poa,nilipokuwa kijana na balehe nilikuwa napenda sana wasichana, yaani nilikuwa natamani sana wanawake wazuri wote wawe wangu, siku mmoja niliposafiri kwenda kijijini kwetu, nikakutana na vijana wa kule kijijini tulikuwa tunapiga story kuhusu mambo ya wasichana, ndipo tukafikia hizo story za kutumia madawa kuwavutia wanawake ndipo kijana mmoja akaniambia babu yake ana dawa nzuri sana ya hizo mambo.

Kwa vile kipindi kile nilikuwa napenda sana wasichana nilimwambia anipeleke kwa babu yake nikachukue hiyo dawa, nilipofika kule nikamwambia yule babu shida yangu ya kupata dawa ya mvuto kwa wasichana, yule babu akaniambia ana dawa mbili ya kuoga na ya hirizi nichague ipi, nikachagua ya hirizi, akaniambia natakiwa nimeze hiyo hirizi ndogo na akanipa na dawa ya maji ninywe ikiwa imechanganywa na damu sijui ni ya mnyama gani.

Baada ya kumeza hirizi na kunywa ile dawa ya maji, yule babu akaniambia kuanzia siku hiyo hakuna mwanamke atakaye nikataa nikimtongoza. Sasa imepita miaka kumi na moja, sijawahi kukataliwa na mwanamke yoyote niliyemtongoza na nimeshakula pesa za wanawake wengi.

Sijawahi kumuomba hela mwanamke akaninyima labda asiwe nayo. Sasa hivi juzi kati, dada yangu nae ameanza kunitongoza anadai anavutiwa na mimi kimapenzi, anasema amevumilia sana ameshindwa imebidi aniambie, najaribu kumuepuka lakini wapi.

Jamani hii dawa inanitesa sana, najuta kuitumia. Imenifikisha pabaya.

Naombeni ushauri wenu.

About the author

kidevu

Leave a Comment