HABARI

Magufuli: Atahadharisha kutofanya safari za lazima kuepuka virusi vya corona

                         Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli

                                                Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani.
Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana kuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania hii leo jijini Dar Es Salaam.
Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo.
”Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.”
”Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua, na hatua zimeanza kuchukuliwa Waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua”.
”Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga na tatizo hili.”
kwa wale wanaopenda kusafiri safiri sana kama safari si ya lazima usisafiri, lazima kuwe na sababu ya lazima ya kusafiri. umefika wakati wa kudhibiti safari zetu kwa ajili ya kujilinda na tatizo hili.
”Zile tahadhari tunazopewa tusizipuuze, ni vyema kuchukua tahadhari, kila mmoja kwenye familia yetu tutoe tahadhari na elimu, mashuleni, vyuoni, makambini, jeshini kwenye magari, tuweze kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu”.
Vyombo vya habari, nyumba za starehe, nyumba za ibada vimetakiwa kuwa na utaratibu wa kuwa na angalau maneno mawili ya kusema kutoa elimu kuhusu virusi vya corona kila wakati.
Kuahirishwa kwa safari za ndege kwenda India
Rais Magufuli amesema kuwa katika hatua ya kudhibiti kuingia kwa maambukizi ya virusi nchini Tanzania, nchi hiyo pia inapunguza taratibu za safari.
amesema ndege iliyokwenda India jana ikirejea nchini Tanzania haitafanya safari tena, kutokana na hali ya nchi mbalimbali kujiweka katika karantini.Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.
      Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.

Nchini Kenya
Kisa cha kwanza cha virusi vya corona Kimethibitishwa nchini Kenya. Waziri wa afya nchini humo Mutahi Kagwe amethibitisha kisa hicho katika tangazo alilolitoa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.
Bwana Mutahi amesema kwamba mtu mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku.
Waziri huyo amesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China.
Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasili nchini humo kutoka Marekani kupitia mjini London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.
Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya.
Hatahivyo waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.
”Tarahe 5 mwezi Machi aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwilini.”, amesema Waziri Kagwe.Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kilithibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumanne
Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kilithibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumanne
Kisa cha pili cha maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus kimethibitishwa nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Mtu huyo anadaiwa kuwa raia wa Cameroon aliyewasili nchini humo kutoka Ufaransa kulingana na mwandishi wa BBC mjini Kinshasa .
Kwa sasa amelazwa hospitalini kwa matibabu. Wizara ya afya nchini humo imetoa wito kwa raia kuzingatia usafi wakati wowote.
Mgonjwa huyo ni raia wa umri wa miaka 46 ambaye anaishi DR Congo na familia yake .
Alirudi nchini humo kutoka Ufaransa mwezi Mei 8 na hakuonyesha dalili za virusi hivyo.
Mamlaka ya DR Congo inasema kwamba kufikia sasa imewatambua watu 117 waliogusana na wagonjwa wawili wa virusi hivyo.
Habari hiyo inajiri siku moja baada ya madaktari nchini DR Congo kuamua kurudi kazini wakisitisha mgomo wa miezi miwili.

Mwandishi wa BBC anasema kwamba muungano wa madaktari ulikubaliana na serikali kuimarisha mazingira yao ya kazi.Ramani inayoonyesha nchi zilizoathiriwa na coronavirus

About the author

kidevu

Leave a Comment