Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.
Kisa cha kwanza cha virusi vya corona Kimethibitishwa nchini Kenya. Waziri wa afya nchini humo Mutahi Kagwe amethibitisha kisa hicho katika tangazo alilolitoa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.
Nchini Ethiopia mamlaka za nchi hiyo pia imetangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya coronavirus. Mgonjwa wa Ethipia ni raia wa Japan.
Bwana Mutahi amesema kwamba mtu mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku.
Waziri huyo amesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China.
Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasili nchini humo kutoka Marekani kupitia mjini London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.
Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya.
Hatahivyo waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.
”Tarahe 5 mwezi Machi aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwilini.”, amesema Waziri Kagwe.
Waziri huyo amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuacha wasiwasi.
Amesema kwamba serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha kwamba hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.
Kamati ya dharura ilioanzishwa ili kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona itaendelea kutoa muongozo ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
Amewahakikishia Wakenya kwamba Kenya imejiandaa vilivyo kukabiliana na virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kitangazwe nchini China, akiongezea kuwa serikali itatumia raslimali zake zote kukabiliana na janga hili.
Amesema kwamba tayari serikali imetambua maeneo yote ambayo muathiriwa alipitia kabla ya kufanyiwa vipimo.
”Mtu anapoambukizwa huhisi maumivu machache na kupona kwa urahisi lakini virusi hivyo vinaweza kuwaathiri zaidi watu wengine hususan wazee na wengine wenye magonjwa sugu”.
Kutokana na hatua hiyo serikali imevunja sheria ya maeneo ya umma na kuwataka Wakenya kufuata maagizo yafuatayo.
1. Kunawa mikono mara kwa mara.
2. Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya – simama umbali wa mita moja
3. Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi ya watu
4.Hakikisha kwamba unaziba pua na mdomo unapokohoa kwa kutumia kitambaa ama tishu.
5. Mtu anayehisi joto ama tatizo la kupumua ametakiwa kusalia nyumbani.
6. Tumepiga marufuku mikutano ya aina yote ikiwemo ile ya umma kama vile ya kidini, michezo, na wanaotaka kwenda makanisani na msikitini watalazimika kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia katika sehemu hizo.
7. Michezo yote inayohusisha shule imepigwa marufuku lakini shule zote zitasalia wazi kwa wakati huu.
8. Wachukuzi wa umma wametakiwa kuhakikisha kuwa abiria wanaosha mikono yao kabla ya kuingia katika magari hayo.
9. Amewaonya Wakenya kutosambaza habari za uongo kuhusu virusi hivyo katika mitandao ya kijamii ambazo zinaweza kusababisha hofu.
10. Wakenya wamewekewa zuio la kutoka nje ya nchi isipokuwa wale wenye umuhimu mkubwa wa kusafiri na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuelekea katika mataifa yenye visa vingi vya ugonjwa huo.
11. Serikali imesema kwamba itatoa maelezo kuhusu ugonjwa huo kila siku.
Waziri huyo amesema kwamba Kenya inaelekea katika wakati ambapo sekta za kibinafsi na zile za kibiashara zitalazimika kuisaidia serikali na raia katika kuchukua jukumu la kukabialana na janga hili.
Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 13 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
Jumla ya visa vilivyothibitishwa | Jumla ya vifo |
---|---|
138,295 | 5,100 |
Visa | Vifo | |
---|---|---|
Uchina | 80,945 | 3,180 |
Italia | 15,113 | 1,016 |
Iran | 11,364 | 514 |
Korea Kusini | 7,979 | 66 |
Uhispania | 4,334 | 122 |
Ujerumani | 3,156 | 7 |
France | 2,879 | 61 |
Marekani | 1,268 | 33 |
Uswizi | 1,125 | 7 |
Sweden | 809 | 1 |
Netherlands | 804 | 10 |
Uingereza | 798 | 11 |
Denmark | 785 | |
Norway | 750 | |
Mili ya Diamond Princess | 696 | 7 |
Japan | 639 | 16 |
Belgium | 556 | 3 |
Austria | 302 | 1 |
Qatar | 262 | |
Malaysia | 197 | |
Bahrain | 189 | |
Singapore | 187 | |
Canada | 157 | 1 |
Israel | 157 | |
Finland | 155 | |
Brazil | 151 | |
Ugiriki | 133 | 1 |
Jamuhuri ya Czech | 117 | |
Ureno | 112 | |
Iceland | 103 | |
Slovenia | 89 | |
Milki za Kiarabu | 85 | |
India | 81 | 1 |
Misri | 80 | 2 |
Kuwait | 80 | |
Iraq | 79 | 8 |
Lebanon | 77 | 3 |
Thailand | 75 | 1 |
Ireland | 70 | 1 |
Romania | 70 | |
San Marino | 69 | 5 |
Indonesia | 69 | 4 |
Saudi Arabia | 62 | |
Poland | 58 | 1 |
Ufilipino | 52 | 5 |
Taipei ya China | 50 | 1 |
Vietnam | 47 | |
Urusi | 45 | |
Chile | 43 | |
Estonia | 41 | |
Ukingo wa Magharibi | 35 | |
lbania | 33 | 1 |
Croatia | 31 | |
Serbia | 31 | |
Slovakia | 30 | |
Belarus | 27 | |
Panama | 27 | 1 |
Algeria | 26 | 2 |
Luxembourg | 26 | |
Georgia | 24 | |
Afrika Kusini | 24 | |
Bulgeria | 23 | 1 |
Costa Rica | 23 | |
Peru | 22 | |
Argentina | 21 | 1 |
Kashmir inayotawaliwa na Pakistan | 21 | |
Cyprus | 19 | |
Hungary | 19 | |
Oman | 18 | |
Ecuador | 17 | |
Latvia | 17 | |
Azerbaijan | 15 | 1 |
Colombia | 13 | |
Bosnia na Herzegovina | 13 | |
Mexico | 12 | |
Malta | 12 | |
Brunei Darussalam | 11 | |
Armenia | 8 | |
Jamaica | 8 | |
Maldivers | 8 | |
Macedonia Kaskazini | 7 | |
Afghanistan | 7 | |
Tunisia | 7 | |
Lithuania | 6 | |
Morocco | 6 | 1 |
Guiana ya Ufaransa | 5 | |
Cambodia | 5 | |
Sri Lanka | 5 | |
Jamuhuri ya Dominica | 5 | |
Paraguay | 5 | |
Kisiwa cha Reunion | 5 | |
Senegal | 5 | |
New Zealand | 5 | |
Liechtenstein | 4 | |
Bangaldesha | 3 | |
Cuba | 3 | |
Visiwa vya Faroe | 3 | |
Moldova | 3 | |
Martinique | 3 | |
Ukrain | 3 | 1 |
Saint Martin (Eneo la Ufaransa) | 2 | |
Burkina Faso | 2 | |
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo | 2 | |
Honduras | 2 | |
Kazakhstan | 2 | |
Cameroon | 2 | |
Monaco | 2 | |
Guernsey | 2 | |
Nigeria | 2 | |
Uturuki | 2 | |
Bolivia | 2 | |
Andorra | 1 | |
Australia | 1 | |
Saint Barthélemy | 1 | |
Bhutan | 1 | |
Vatican | 1 | |
Visiwa vya Cayman | 1 | |
Ethiopia | 1 | |
Gabon | 1 | |
Gibraltar | 1 | |
Guinea | 1 | |
Guadeloupe | 1 | |
Guyana | 1 | 1 |
Jordan | 1 | |
Kenya | 1 | |
Mongolia | 1 | |
Nepal | 1 | |
Sudan | 1 | 1 |
Togo | 1 | |
Trinidad and Tobago | 1 | |
Cote d’voire | 1 |
Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo
Mara ya mwisho kufanyiwa mabadiliko 13 Machi 2020, 18:30 GMT +1.
Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 13 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
Jumla ya visa vilivyothibitishwa | Jumla ya vifo |
---|---|
138,295 | 5,100 |
Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo
Mara ya mwisho kufanyiwa mabadiliko 13 Machi 2020, 18:30 GMT +1.