HABARI

Magereza watoa ufafanuzi kuhusu wafungwa kunyanyaswa gerezani

Jeshi la Magereza nchini limetoa ufafanuzi kuhusu madai ya viongozi wa CHADEMA kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili gerezani na kusema kuwa tuhuma hizo si za kweli.

Msemaji huyo ameeleza kuwa mambo mengi waliyozungumza ni utaratibu wa kawaida ambayo mfungwa au mahabusu anapaswa kufuata muda wote akiwa gerezani.
Ufafanuzi huo unatolewa na msemaji wa jeshi hilo Mrakibu Mwandamizi Amina Kavirondo wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.
Kavirondo amesema jukumu la Magereza ni usalama wa mfungwa, mtu mwingine yeyote anayeingia gerezani lazima akaguliwe na jambo hilo linafanywa ili kuepuka njia mbalimbali za kupata vitu hatarishi bila kuzingatia wadhifa au ni nani anaingizwa gerezani.
Amesema mahabusu wote wanapaswa kufuata sheria za magereza hasa zinazohusu usalama wake na watu wengine.
Kuhusu kufanya kazi gerezani amesema ni utaratibu wa kawaida wa urekebishaji wa tabia kwa mfungwa kwani viongozi hao tayari walishakuwa wafungwa.
Kuhusu kupima HIV hadharani msemaji huyo ameeleza kuwa viongozi hao walipimwa vipimo vyote ikiwemo HIV na kifua kikuu ili kujua mwenendo wa afya zao utaratibu ambao unatumika kwa wafungwa wote ili kupata huduma maalum zinazostahili endapo wakikutwa na ugonjwa kwa kipindi chote wakiwa gerezani.

About the author

kidevu

Leave a Comment