Mshambuliaji wa zamani wa Man United anayeichezea club ya Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameweka wazi kuwa kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alimtaka asiondoke katika club hiyo ili aendelee kuitumikia Man United.
“Ilikuwa ni hali ngumu kwangu na nilitakiwa nifanye maamuzi ya kwenda sehemu ambayo naweza kujifunza vitu vingine kuhusiana na uchezaji wangu na kufanya kazi na mtu ambaye ananihitaji, Ole alinitaka nibaki lakini nilimwambia kuwa nimemaliza”>>>Lukaku
Lukaku aliondoka Man United 2019 baada ya kukaa katika club hiyo kwa miaka miwili lakini hakuwa na wakati mzuri sana kama ilivyokuwa kwa Inter Milan, Lukaku aliishawishi Man United imsajili 2017 kufuatia kiwango chake cha kucheka na nyavu alichokionesha Everton lakini ikawa tofauti akiwa Man United.