HABARI

LaLiga yasimamishwa kwa muda usiojulikana

Shirikisho la soka Hispania (RFEF) limetangaza kuwa limesitisha michuano yote ya soka nchini Hispania ikiwemo LaLiga kwa muda usiojulikana.
RFEF wanasema watarejesha tu michuano hiyo kama mamlaka zitajiridhisha kuwa ni wakati salama kwa afya za watu.
Awali LaLiga ilisimamishwa hadi mwanzoni mwa April lakini sasa imeonekana hali kutokuwa nzuri katika mapambano na virusi vya corona, hivyo hawezi kuruhusu mechi ziendelee.

About the author

kidevu

Leave a Comment