HABARI

“EX Wangu Alinishauri Niwe Kama Mwanamke”- Makabila

Mkali wa singeli Dulla Makabila, amenyoosha maelezo kwa kusema mpenzi wake wa zamani Fia Makabila alishiriki na kutoa wazo la yeye kujifanya kama mwanamke, ila ameshangaa baada ya kuachana naye akaponda wazo hilo.


Dulla Makabila amesema “ex” wake huyo alipenda wazo hilo, ila sasa hivi hawapo wote ndiyo anaponda na binafsi anachukulia kawaida tu kushambuliwa na mpenzi wake huyo wa zamani.

“Tungekuwa kwenye mahusiano asingesema vile, hili wazo nililipata nilipokuwa nipo naye, aliipitisha, alishiriki na alipenda ila kwa kuwa sasa hivi tumeachana ndiyo ame-comment hivyo, kwamba ni kitendo cha kitoto, kushambuliwa na ex wako ni kitu cha kawaida tu kwa sababu hatupo wote na tungekuwa pamoja asingesema hivyo” amesema Dulla Makabila.


Ikumbukwe tu mpenzi wake huyo wa zamani, alisema ameshangazwa na kitendo cha kitoto alichofanya Dulla Makabila kwa kujifanya mwanamke ili kuitangaza kazi yake mpya.

About the author

kidevu

Leave a Comment