Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ameweka wazi kuhusu kile anachokifanya msanii mwenzake wa Bongo Fleva ambaye pia yupo kwenye lebo ya Konde Gang H Baba kuonekana kumkingia kifua sana Harmonize na kufikia hatu hata kuwaongelea watu wengi na kuwakemea pale anapoona wanamuongelea au kumpiga vita Harmonize.
Harmonize ameongea hayo akifanya mahojiano na kituo cha east Afrika Redio na majibu ya Harmonize yalikuwa hivi:”H Baba ni mmoja ya kaka zangu ambaye alinitangulia kwenye sanaa lakini suala na kupost na kufanya nini sijui huwezi kumpangia mtu maamuzi yake ile ni akaunti yake na anachokizungumza anazungumza kitu anachoona yeye kwake ni sahihi, Sasa ukitaka kumpangia mtu kwamba usipost hiki utakuwa kama unamuingilia maisha yake halafu ukiangalia mi mdogo tu nimeanza sanaa juzi tu, Itaonekana mdogo wangu we unanifundisha unajua mi nimepitia machungu mangapi?, Kwahiyo ni mtu ambaye namheshimu na nayaona anayepost kama unavyoona wewe”