HABARI

Wazazi washtakiwa kwa ‘kumruhusu’ mtoto wao kuvalia nguo za kike

                           Luiz katika hafla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni na wazazi wake
             Luiz katika hafla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni na wazazi wake

Luiz ni mtoto wa kiume wa miaka mitano ambaye anapendelea kuvalia mavazi ya kisichana na mapambo yake.
Jina lake na la wazazi wake yamebadilishwa ili kulinda faragha yao wasitambuliwe.
Tangu mwaka 2018, wazazi wake walimruhusu kuvalia kama msichana na kutembea katika barabara za kijiji chao kidogo katika jimbo la Santa Catarina kusini mwa Brazil.
Lakini hatua hiyo haikuchukua muda mrefu, wazazi hao walishtakiwa na mtu asiyejulikana kwa wizara ya wanawake ,familia na haki za binadamu.
Mpigaji simu huyo alisema kwamba Luiz “alishawishiwa na wazazi kuvalia mavazi ya kisichana” na kwamba alikuwa akinyanyaswa na wanafunzi wenzake shuleni.
Kesi hiyo moja kwa moja iliwasilishwa kwa huduma ya mashtaka ya umma.
“Hilo lilikuwa pigo kubwa kwetu. Nadhani hatua hiyo ilikuwa ya kushangaza,” anasema Cesar, baba yake mtoto huyo.

Kubadili nia

Baba huyo ambaye pia ni afisa wa polisi alikuwa tayari amefanya maamuzi kuhusu mtazamo wa suala la jinsia baada ya kijana wake wa kiume kuanza kuvalia mavazi ya watoto wa kike.
“Niliwahi kuwa na tabia ya kuogopa kutangamana na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Lakini nimebadili tabia hiyo,” aliambia BBC.
“Nilijifunza kuwa kuwadhihaki au kutoa kauli ya kuwadhalililisha ni kuwakosea hesima.”Luiz akiwa amevalia ngu ya kischana
                                    Luiz alianza kuvalia ngu za watoto wasichana akiwa na miaka mitatu
Mama yake Luiz, Maria, amabye ametengana na Cesar lakini wanashirikiana kumlea mtoto wao, aliguswa sana na malalamishi
“Ilikuwa hali ngumu sana,”alisema.
“Hofu yangu kubwa ni kwamba mtu atasema kitu kitakachomuumiza.”
Hofu ya Maria iliongezeka wakati familia yao iliposhtakiwa muda mfupi baada ya yeye na Cesar kumruhusu mtoto wao wa kiume Lui kuvalia mavazi ya kike na kutembea mtaani.
Ofisi ya mwendesha mashtaka imeanza uchunguzi kuhusiana na suala hilo. Inahoji kuwa, kwa mujibu wa sheria ya kuwalinda watoto nchini Brazil, haki ya Luiz huenda “imetishwa au kukiukwa”.Luiz anapendelea kutazama vikaragozi, ni moja ya ile nayopenda sana inafahamika kama Frozen
            Luiz anapendelea kutazama vikaragozi, ni moja ya ile nayopenda sana inafahamika kama Frozen
Lakini ilifikia uamuzi kwamba wazazi wa mtoto huyo “Walisisitiza kwamba mtoto wao ndiye anapendelea mavazi ya kischana na marembo yake, bila ya kushurutishwa na mtu yeyote”.
“Hakuna hatari yoyote iliyomkabili Luiz,” waendesha mashtaka waliandika katika ripoti yao
“Tofauti na hali ilivyo, wazazi walionesha ukomavu na kwamba alikuwa tayari kukabiliana na hali hiyo pamoja na mtoto wao, [ambaye] wanamuunga mkono vilivyo.
Kwa hivyo hakuna, ushahidi kwamba haki ya mtoto inakabiliwa na tishio la aina yoyote.”
Kesi hiyo ilifungwa Novemba 27, mwaka 2018. Wazazi wa Luiz hawakuwahi kuwambia kuhusu uchunguzi huo.
“Ni mdogo sana na hivi ni vitu ambavyo kwa mtazamo wetu [hafai] kuambiwa,” Maria alielezea.

Ushauri wa kisaikolojia

Mama yake Luiz anasema mtoto wao anapendelea kuitwa Luiza. Kufuatia ombi la wazazi, ambao wanachukulia suala hilo kuwa katika awamu ya kwanza, taarifa hii inamwangazia Luiz katika jinsia ya kiume.
Lakini Cesar na Maria wanaamini muda ukiwadia atatambulishwa kama msichana.Cesar naLuiz katika picha ya familia
Cesar (kulia) anasema alilazimika kubadili msimamu wake kuhusu masuala ya jinsia kutokana na hali ya mtoto wake
Miaka miwili iliyopita wazazi wake waliamua kutafuta ushauri wa kisaikolojia na kufikia uamuzi kwamba mtoto huyo ana jinsia mbili.
“Hajawahi kusema anataka kuwa na ndevu au kuwa mwanamume ,” Cesar alisema.
“Alianza kuomba kuvishwa kama msichana’ nguo na marembo mengine.”
Afisa huyo wa polisi aliambia BBC kuwa mwanzoni alipata changamoto kumuelewa mtoto, lakini wakati wote alijaribu kuheshimu uamuzi wa mtoto wake.

Hatima ya baadaye

César na Maria hawajaamua jinsi Luiz atakavyofikia mabadiliko hayo ya jinsi.
Wanaamini katika kipindi cha miaka michache ijayo mtoto wao ataonelea haja ya kubadili jinsia yake na kupewa matibabu ya homoni.
“Lakini bado hatujatafikiria jinsi tutakavyofanya hilo,” Cesar alisema.Luiz akipimisha nguo
Luiz alianza kuomba kuvishwa mavazi ya wasichana akiwa na miaka mitatu

Ni kwasababu niko tofauti. Nilizaliwa mvulana, lakini mimi ni msichana.
LuizLuizna na Cesar
“Baadhi ya watu walifikiria nitakuwa na haya kuhusu suala la mtoto wangu, nimemkubali jinsi alivyo,” Baba yake ya Luiz

Katika mazungumzo mafupi na BBC, Luiz alisherehekea anasherehekea kuwa wajomba Wake wameanza kumkubali jinsi alivyo.
“Ananiunga mkono,” alisema kijana huyo kuhusu jama zake ambao, kwa mujibu wake, ni mpenda dini na mwanzoni alikuwa haelewi kwanini mtoto anavalia mavazi ya kike.
Ni kwasababu mimi ni tofauti
Luiz anafahamu kuwa watu wanatatizika kuelewa uamuzi wake.
“Ni kwasababu mimi ni tofauti. Nilizaliwa mvulana, lakini mimi ni msicahana.” alisema, kwa uwazi.
“Lakini hilo sio tatizo,” Luiz aliongeza
Mwaka 2020 mtoto huyo anataka kufikia ndoto aliyokuwa nayo kwa miaka miwili: ya kuvalia sketi kama sehemu ya sare zake za shule.
“Naamini huu ndio wakati,” baba yake alisema
Ni mtoto mzuri na mwerevu. Nijivunia sana binti niliye naye.

About the author

kidevu

Leave a Comment