HABARI

Julian Peters: Mwanamke aliyezaliwa bila uke wala mfuko wa uzazi

Julian Peters
                      Tatizo la Julian Peters halina tiba zaidi ya kukubali hali yake.

Julian Peters ni mwanamke wa miaka 29 aliyezaliwa na ugonjwa unaojulikana kama (MRKH) Mayer-Rokitansky-Küster-Hauser, huu ni ugonjwa unaoathiri sana wanawake na hasa kizazi cha mwanamke. Hali hii inamaanisha kuwa Julian alizaliwa bila mfuko wa kizazi.
“Hali hii ninayoishi nayo inachangamoto nyingi kwani kila siku ninakabiliana na hisia mseto, mbali na hayo jamii inayonizunguka pia wakati mwengine inataswira tofauti kuhusu hali hii”, anasema Bi Julian
Julian anasema kuwa maoni ya jamii yanatofautiana kuhusu hali yake kwani kuna wale ambao wanaamini kuwa hali anayoishi nayo sio ugonjwa bali ni jambo aliliojiletea mwenyewe, pengine kwa dhana kuwa aliavya mimba nyingi au pengine aliwahi shiriki maswala ya ushirikina.
Julian anasema maoni hayo wakati mwengine yanakera lakini anavumilia na kuendelea na maisha yake.
Aligundua kuhusu ugonjwa huu akiwa kidato cha tatu, wakati huo alikuwa na miaka 17, anakumbuka alikuwa alienda nda hospitalini kupata ushauri wa daktari kwa sababu alikuwa anaumwa na miguu yake. Alipofika hospitalini dakatari alianza kwa kumuuliza baadhi ya maswali
“Daktari aliniuliza wakati wa mwisho wa kupata hedhi yangu ni lini? Jibi langu lilikuwa sikuwa nimepata hedhi zangu” Julian akasema.Kulingana na daktari Mutindi Kakuti wanawake wenye ugonjwa huu wanaweza kushiriki ngono endapo watafanyiwa upasuaji wa kurekebisha njia au sehemu siri ya kike
Kulingana na daktari Mutindi Kakuti wanawake wenye ugonjwa huu wanaweza kushiriki ngono endapo watafanyiwa upasuaji wa kurekebisha njia au sehemu siri ya kike
Baada ya daktari aliyekuwa anamtibu kufahamu kuwa kwa umri wake Juliana wa 17 hakuwa na hedhi, dakatari alitaka afanyiwe uchunguzi wa sehemu zake za uzazi, baada ya uchunguzi kufanywa ikiwa ni pamoja na kupigwa picha ya kizazi chake, hapo ndipo iligunduliwa kwamba alikuwa hana kizazi chote kama wanawake wengine na pia njia ya uke wake ilikuwa imeziba kutoka upande wa nje.
Japo alikuwa hana umri mkubwa sana hakuelewa mengi kuhusiana na hali hiyo, kwa hiyo alipoelezwa na dakatari kama binadamu hakuamini alichokuwa anaelezwa, Julian anasema.
“Wakati huo nilikuwa shuleni na nilikuwa tayari nasomea baiolojia, nilifahamu jinsi mwili wa mwanamke unavyopaswa kufanana, kwa hiyo nililia sana kwa kutambua kuwa sehemu ya kizazi changu zilikuwa na kasoro ila sikuwa na lingine la kufanya”
Madaktari wakati huo waliamua kuwa wangemfanyia upasuaji ili kufungua njia ya uke wake.
Japo katika suala la mfuko wa kizazi hakuwa na la kufanywa zaidi ya kukubali kuishi maisha yake hivyo.
Juliana anasema kuwa “Nilikubali kuhusu hali yangu nikiwa umri wa miaka 24, baada ya kuelezwa ukweli wa mambo, nilirejea shuleni tu na kuamua kusoma kweli kweli. Nilipomaliza shule ya sekondari nilianza kufanya uchunguzi wangu vitabuni, na nikaanza kuelewa changamoto nilizokuwa napitia kama muathiriwa wa ugonjwa huu”Julian Peters
Mwanamke mmoja kati ya 4000 ulimwenguni ana tatizo la kutokuwa na kizazi sawa na la Julian
Julian anasema amekuwa na mahusiano ya kimapenzi, lakini hajajihusisha na shughuli ya ngono kwani kwake kila daraja ambalo anavuka maishani mwake anahitaji kujitayarisha na kuwa makini zaidi lakini haijakuwa rahisi.
Anasema kama ilivyo kawaida mahusiano ya kimapenzi huhusisha wapenzi kuzungumza na kuwa wazi, lakini kwake pale anapowaeleza wapenzi wake kuhusu hali yake, uhusiano huo unafikia mwisho.
“Wajua mtu ana haki ya kuwa na wewe au la, kwa hiyo mimi ninaelewa pale mpenzi wangu au mtu ambaye niko naye anaponieleza kwamba uhusiano wetu hauwezi kusonga mbele”Julian alisema.
Upasuaji wa mwisho Julian anasema ulihusisha kufanyiwa marekebisho kwenye uke wake sio kwa sababu ya kujifungua mtoto, lakini aweze kushiriki ngono.
Anasema kuwa bado hajaamua kuanza tendo lenyewe kwani matumaini yake ni kupata mtu ambaye atamkubali alivyo kwanza.
Julian anasema kuwa huenda swala la kuwa hataweza kushika mimba maishani mwake huwafukuza wanaokuwa na nia ya kumchumbia ila hajakata tamaa ya kuwa na mtoto.
“Sio lazima uwe mama kwa njia ya kuzaa pekee yake unaweza kuamua kumrithi mtoto ambaye hana wazazi na kumlea kama wako.” Julian amesema.
Kulingana na daktari Mutindi Kakuti, maswala ya uzazi nchini Kenya, hali hii hutokea wakati mtoto wa kike anapokuwa tumboni mwa mama yake, na wakati mwengine huibuka kuwa viungo vya mwili hususan vya uzazi vya mtoto hukosa kujiunda kama inavyofaa au kama ilivyokawaida.
Daktari Kakuti anasema kuwa kiini haswa sio kwamba huu ni ugonjwa wa kurithishwa kutoka kwa mama hadi mtoto au kutoka kwa ukoo, ila tu ni jambo ambalo linaweza kufanyika kwa yeyote na inasemekana kati ya wanawake 4000 ulimwenguni mmoja huenda akawa na tatizo hili.
Kulingana na daktari Kakuti wanawake wenye ugonjwa huu wanaweza kushiriki ngono endapo watafanyiwa upasuaji wa kurekebisha njia au sehemu siri ya kike. Lakini baada ya upasuaji huo, huenda ukahisi uchungu mwingi wakati wa kuanza tendo hilo.
Japo anasema kuwa wanawake wenye ugonjwa huu hawawezi kupata watoto kwani hawana mfuko wa kizazi, kutokana na utafiti wa kisayansi ambao upo karne hii mwanamke anaweza kubebewa mtoto na mwanamke mwengine mchakato unaojulikana kwa kiingereza kama (Surrogate mothers ).

About the author

kidevu

Leave a Comment