Saren Idaho (kushoto) na Prince Latoya walizuiliwa kwa miezi mitano gerezani katika mji wa Sierra Leone
Saren Idaho anasema hajawahi kwenda Sierra Leone wala hajawahi kuwa nchini humo hadi alipohamishwa huko kutoka Marekani miezi sita iliyopita.
“Sina ninayemfahamu hapa,” analalamika baba wa watoto wawili, 55.
Akionekana mgonjwa na mwenye kutaabika hata anaotembea, aliketi kwenye kiti ch aplastiki na chumba cha hoteli mji wa Freetown. Alikuwa anazungumza huku akivuta sigara na kuangusha vipande vya pande kando ya trei iliyokopo pembe yake.
Anasema kwamba afadhali hapo kulikuwa kuzuri zaidi kuliko gerezani ambapo alilala na sakafuni na mende, panya na kunguni kwa miezi mitano ya kwanza alipoingia nchini humo.
Prince Latoya, 47, alikuwa kwenye ndege hiyo hiyo iliyokuwa inafurusha na pia katika hali hiyo hiyo.
Wanaume wote wawili ambao hawakuwahi kujuana hapo kabla ya kuingia Sierra Leone, walikuwa ni wakazi wa kudumu Mareani. Lakini anasema kwamba wao ni kutoka Caribbean, ila mamlaka iliwakana.
Wanaume hao wawili sasa wanaishi kwenye hoteli moja mji mkuu wa Sierra Leone
Idaho na Latoya pamoja na raia 17 wa Sierra Leonean na wengine wa Afrika Magharibi walikuwa wamehukumiwa kwa kufanya uhalifu Marekani.
Waliishia kuingizwa kwenye ndege ya kuwarejesha nyumbani baada ya ubalozi wa Sierra Leone mjini Washington DC kupata shinikizo kutoka kwa maafisa wa Marekani kulingana na Isha Sillah, mkuu wa maeneo ya Marekani na Pasifiki katika wizara ya nje.
Anasema kwamba mamlaka ya Uhamiaji Marekani iliwasilisha nyaraka katika ubalozi na kusemekana kwamba wanaume hao wawili ni raia wa Sierra Leone. Bila ya nyaraka zao kupitiwa tena, maafisa wa ubalozini waliwapa vyeti vya dharura vya kusafiria.
Ubalozi ulisema kwamba kile kilichofanya wao kuchukua hatua kama hiyo, ilikuwa ni shinikizo kutoka kwa Idara ya Uhamiaji na mambo ya ndani ya kuwakubali kama raia wa Sierra Leoneon.
“Serikali ya Sierra Leone ni kama kibaraka kwa Marekani,” Latoya, ambaye alisema yeye ni raia wa Bahamas, amezuiambia BBC.
Idaho alikasirishwa sana na mamlaka ya Marekani.
“Marekani ilighushi nyaraka ili kunileta mimi hapa na kudai kwamba hii ni nchi yangu,” amesema. “Na mimi mwenyewe ninajua kwamba sikuzaliwa katika nchi hii.
“Mimi ninatoka Dominica. Kipi kinafanya iwe vigumu kurejea Marekani?”
‘Alikataliwa na Dominica’
Hili limekuwa tatizo kubwa la ukiritimba.
Wizara ya mambo ya nje imewasiliana na balozi za nchi mbili za Caribbean mjini Washington kuthibitisha kwamba wanaume hao wawili ni raia wa nchi hizo.
“Ubalozi wa Dominican umekanusha kwamba Idaho ni raia wake huku ubalozi wa Bahamia ukisema kuwa nyaraka zaidi zinahitajika ili iweze kufanya maamuzi, ”amesema Bi. Sillah.
Lakini hadi kufikia sasa wamekwamba katika hotelini.
Idaho, akiwa amepigwa picha na mtoto wake miaka 10 iliyopita, anataka kuungwanishwa tena na familia yake
Maneja, Osman Kamara, alisema kwamba wawili hao walitafutiwa hoteli hiyo na polisi lakini gharama ya kulipia chumba hicho ikawa juu nusura wafurushwe kabla ya msamaria mwema ambaye ni mfanyabiasha kuamua kuwalipia.
Pia aliwalipia chakula na kuwapa pesa za kununua nguo.
Kabla ya hapo kila mmoja wao alikuwa anapokea $2.50 (£2) kugharamia mahitaji yao ya kila siku lakini ambazo walisema ziliweza kununua kiamsha kinywa na chupa ya maji ya kunywa pekee
“Tumekuwa tukiishi bila chakula, matibabu, yaani bila chochote,” amesema Latoya.
Wanaume hao wawili wamekuwa wakipokea pesa wanazotumiwa na jamaa zao kupitia Western Uion. Lakini stakabadhi za usafiri za Sierra Leone kwa sasa wakati wake umeisha na hawawezi tena kupokea pesa kwasababu wanahitajika kuwa na kitambulisho.
Idaho anasema kwamba amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 28 hadi alipokamatwa na kufungwa jela 2018 kwa makos aya kuendesha gari akiwa mlevi.
Alipoteza vitambuisho vyakwe vyote. Walikuwa kwenye nyumba ambayo ilichukuliwa na benki na akashindwa kuendelea kuilipia kwasababu alikuwa gerezani, amesema.
“Stakabadhi zangu zote, pamoja na vyeti vya kuzaliwa, zimefungiwa katika chumba kimoj abadaya kushindwa kulipia nyumba niliyokuwa ninainunua,” ameiambia BBC.
Mowanda Idaho anasema kwamba vijana wake wawili wanamtamnani babayao
Mke wake wa miaka 17, Mowanda Idaho, na vijana wake wawili,wa miaka 14 na 11, kwasasa wanaishi Marekani jimbo la South Carolina.
“Tumekuwa na hali ya kukatisha tamaa kabisa kati yangu mimi na kijana wangu, 14, ambaye kwasasa amepata msongo wa mawazo na kushindwa kwenda shule,” Bi. Idaho, ambaye ni raia wa Marekani, amesema hivyo kwa njia ya simu.
Mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kwa dakika tano tu akiwa gerezani Aprili 2018.
Mke wake anasema amezungumza na wakili ya uhamiaji lakini hana pesa za kshtaki serikali.
Latoya, ambaye ameeishi Marekani kwa miaka 25, alihukumiwa kwa wizi. anasema yeye hana watoto wala mke.
‘Walisema kwamba wanatoka Sierra Leone’
Lakini serikali ya Marekani ina mtazamo tofauti.
Kupitia barua pepe iliyoandikiwa BBC, wizara ya mambo ya ndano imemuelezea Latoya kama ”raia wa kigeni mhalifu ambaye ameshtakiwa kwa makosa kadhaa yenye kuhusishwa na uhalifu”.
Wizara hiyo inasema kwamba aliingia nchi humo mwaka 1997 kwa njia haramu na mara kadhaa, Latoya amekuwa akiwaambia maafisa wa Uhamiaji wa Marekani kwamba yeye ni raia wa Sierra Leone”.
Aidha ubalozi wa Sierra Leonean mjini Washington umethibitisha kuwa yeye ni raia wake.
Latoya amekanusha kabisa kuwa aliwahi kusema yeye anatoka Sierra Leone.
“Sikuwahi kuwambia kwamba mimi ninatoka Sierra Leone,” amesema.
“Sijui taarifa hii waliipata wapi. Niliingia Marekani kwa kutumia boti kutoka Bahamas. Niliwaomba wao kutoa ushahidi wowote unaoonesha kwamba mimi ni raia wa Sierra Leone.”
Mamlaka ya Marekani pia imemuita Idaho “raia wa kigeni mhalifu”, aliyeingia nchini humo 1999, na kuongeza kwamba alikuwa ameshtakiwa mara kadhaa kwa kuendesha gari akiwa mlevi”.
“Sikuwahi kusema kwamba mimi ni raia wa Sierra Leone,” Idaho amesema. “Mimi sina rekodi yoyote ya uhalifu. Nimeshtakiwa mara moja tu kwa kuendesha gari nikiwa mlevi.”
Pia Sierra Leone ina historia ya kukataa kutoa stakabadhi za usafiri kwa raia wake hali inayoweka nchi hiyo kuwa katika kundi la nchi zenye kupata visa za muda mfupi tu za kuingia Marekani kulingana na vikwazo vya 2017.
Wakisubiri kupata stakabadhi za usafiri
Lakini serikali haina uhakika kwamba wanaume hawa wanatoka Sierra Leone. Ilitaka kuwasafirisha wanaume hao wawili hadi Caribbean ila kwasababu ya ukosefu wa uthibitisho wa uraia wao, kwasasa inatumai kwamba itafanikiwa kuwakabidhi katika ofisi ya kimataifa ya uhamiaji (IOM).
Mkuu wa IOM, Sierra Leone, Sanusi Savage, amesema shirika lake halijapokea ombi rasmi zaidi ya simu kutoka wizara ya mambo ya nje akiwemo waziri, Nabilla Tunis, akiomba usaidizi.
“Niliahidi kutoa msaada wa tiketi lakini baada ya wao kuthibitisha stakabadhi rasmi za usafiri na kukubaliwa na nchi zao,” ameiambia BBC.
Lakini hilo bado halijatokea.