Siku ya jana ya tarehe 12/3/2020 Waziri wa Nishati hapa nchini Tanzania Dkt.Merdad Kalemani alifanya ziara ya kushtukisha katika mradi wa umeme wa Rea wilayani Ilala ambapo alitemebea maeneno ya Majohe na kukuta nguzo zenye zaidi miezi kadhaa zikiwa zimelele chini na nyingine ambazo zimechimbiwa zikiwa bado hazijaunganishwa umeme na baadhi zikianza kuaharibika.
Baada ya kutembelea maeneno hayo alikuta hali sio nzuri kwa wakazi wa Maeneo hayo kwani hakuna kitu kilichofanyika huku wananchi wakiendelea kupata shida haliyakuwa nguzo zimechimbiwa kabisa lakini tatizo ni kuunganishiwa umeme
Mbali na maeneo mengine kuwa na nguzo lakini sehemu zingine hakukuwa na nguzo kabisa na badala yake yalitakiwa ywe tayari yamechimbiwa nguzo.
Baada ya kukagua maeneno hayo na kunyesha kutoridhishwa na mwenendo wa mradi huo alitoa siku moja katika baadhi ya meneo umeme uwe umeshawaka lakini katika maeneo yote yaliyotakiwa kupitiwa na umeme mpaka tarehe 30/3/2020 kila nyumba iwe na umeme.
Waziri alimtaka meneja mwadamizi wa TANESCO kanda ya Kisarawe na Pwani Mhandisi Nyanda kuachia ngazi endapo Umeme hautawaka siku ya leo maeneno ya Majohe baada ya meneja huyo kuahidi kuwa ifikapo leo baadhi ya maeneo umeme utaanza kuwaka.