Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi kuacha kuingiza nyaya na matransifoma kinyemera na badala yake wanatakiwa kutumia zinazotengenezwa hapa nchini.
Alisema kuwa tunafanya ufatiliaji kwa wakandarasi wanaoingiza bidhaa hizi kinyemera endapo akigundulika atahesabika in moja kati ya watu wanaohujumu uchumi.
Akizungumza na waandishi jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifanya ziara yake katika kiwanda cha Tropical Industries Dkt Kalemani alisema kuwa kumekuwa na udanganyifu unaofanywa na wakandarasi kusema kuwa hakuna nyaya, Transifoma vifaa vya kuwekea umeme vijijini. “Leo nimekuja kiwandani nimejionea transfoma na nyaya wakandarasi wanachelewa wakati vifaa vipo wanaonyesha hali ya kujichelewesha kuna mahali wanataka kwenda kuchukuwa na sisi hatutaki bidhaa kutoka nje” “Silazimishi wachukuwe kwenye hapa wachukuwe popote lakini isiwe nje ya nchi, kowanda hiki kina transifoma 75 elfu wakati wakandarasi wanasema kuwa hazipo wakati zipo za kutosha” “Vifaa vya ndani vinatosha lea ilikuwa ni huhitaji mkubwa sana Mahitaji yetu ya ndani ni transifoma 21 elfu tunazonyingi na zakutosha, pamoja na nyaya za kutosha zipo”