HABARI

Coronavirus: Je Covid-19 inavyoweza kuathiri mipango ya matamasha

Diamond Platnum alikua amepanga kufanya safari zake katika mataifa mbali mbali, lakini kutokana na janga la coronavirus huenda akalazimika kuyaahirisha

     Diamond Platnum alikua amepanga kufanya safari zake katika mataifa mbali mbali, lakini kutokana na janga la coronavirus huenda akalazimika kuyaahirisha


Mlipuko wa virusi vya corona ambao umesambaa katika mataifa mbali mbali duniani unaonekana kuathiri matukio mbali mbali zinayohusisha mikusanyiko ya watu, miongoni mwa shughuli hizo zikiwa ni matamasha.
Nasib Juma al maarufu Diamond Platnum kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram ametangaza kuwa kutokana na Coronavirus ameahirisha Matamasha yake ya Ulaya na kwamba tarehe ya matamasha hayo itatangzwa karibuni:
Awali Diamond alikua amewaalika wapenzi wa muziki wake kuhudhuria matamasha yake mkiwemo tamasha ambalo alitarajia kulifanya nchini Uswiss, ambapo akiwahamasisha kununua tiketi za tamasha mapema:
Ruka ujumbe wa Instagram wa diamondplatnumz

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa diamondplatnumz
Msanii maarufu wa Nigeria Davido Adeleke pia amelazimika kuahirisha tamasha lake alilotarajiwa kulifanya Marekani kutokana na mlipuko wa Coronavirus. Licha ya kwamba tiketi za tamasha hilo ziliuzwa na kuisha imemlazimu kuwaomba radhi mashabili na wapenzi wa muziki wake:
”Ninasikitishwa na kuvunja kile ambacho kimeshuhudia kuuzwa kwa tiketi zote za safari bora ya kimuziki hadi sasa , lakini kuahirisha ni kitu sahihi kukifanya. Kwa afya na usalama wa mashabiki wangu na wahudumu ni muhimu na hakuna kingine tena cha muhimu. Uwe salama nitawaona hivi karibuni! Mungu awe nanyi nyote!” ulisema ujumbe wa Davido kupitia mtandao wake wa Instagram
Ruka ujumbe wa Instagram wa davidoofficial

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa davidoofficial
Nchini Kenya pia shughuli mbali mbali zikiwemo zenye mikusanyiko ya watu yakiwemo matamasha zimesitishwa hususan baada ya mtu mmoja kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona Ijumaa.
Moja ya burudani zilisotangaza kuahirishwa ni burudani ya vichekesho inayotolewa kupitia televisheni. Mmiliki wa kampuni ya Churchill Daniel Ndambuki, al maarufu Mwalimu king’ang’i amefuta maonyesho yake kufuatia mlipuko huo katika taarifa yake aliyoituma kwenye ukurasa wake wa Facebook:
Ruka ujumbe wa Facebook wa Daniel “Churchill” Ndambuki aka Mwalimu King’ang’i

Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Daniel “Churchill” Ndambuki aka Mwalimu King’ang’i
Mchekeshaji maarufu wa Televisheni nchini Marekani Trevor Noah ameahirisha kuishirikisha hadhira katika kipindi chake kutokana na hofu ya coronavirus.
Mchekeshaji huyo kutoka kutoka Afrika Kusini Trevor Noah huialika hadhira katika kipindi chake cha kila siku ya Alhamisi kinachopeperushwa moja kwa moja ameambua kuwa hatawaalika watu kuja katika studio yake kutokana na janga la virusi vya corona.
Trevor Noah amesema kipindi chake cha Daily Show kililazimika kutekeleza jukumu lake la kukabiliana na virusi vya corona.
” Kutekeleza sehemu yangu ya kukabiliana na janga, Daily haitakuwa na hadhira ya moja kwa moja studio kuanzia Jumatatu.
Matamasha mengine makuu yamechukua hatua sawa na hiyo huku virusi hivyo vikiripotiwa kusambaa nchini Marekani.
Tayari kuna zaidi ya visa 1,300 vya coronavirus vilivyothibitishwa nchini Marekani, huku vifo 40 vikiripotiwa.

festival stageHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMatamasha mengi ya muziki yameahirishwa katika maeneo mbali mbali duniani

Matamasha mengine makuu yamechukua hatua sawa na hiyo huku virusi hivyo vikiripotiwa kusambaa nchini Marekani.
Tayari kuna zaidi ya visa 1,300 vya coronavirus vilivyothibitishwa nchini Marekani, huku vifo 40 vikiripotiwa.
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita , matamasha makubwa zaidi yameahirishwa kutokana na hofu juu ya virusi vya corona.
Hakuna safari za matamasha kabisa kote barani Asia na Italia kwa sasa, huku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000 ikiahirishwa katika mataifa ya Uswis, Ufaransa na katika baadhi ya miji nchini Ujerumani.
Hakuna matamasha ambayo yamefutwa nchini Uingereza bado, lakini serikali haijazuwia matukio makubwa huku visa vya coronavirus vikiendelea kuongezeka.
Kufutwa kwa mikusanyiko na matamasha mbalimbali kunatarajia kusababisha hasara katika sekta ya burudani kwa watu na makampuni binafsi katika maeneo mbali mbali duniani.

About the author

kidevu

Leave a Comment