HABARI

Golikipa wa Aston Villa ajihofia kuwa na corona

Golikipa wa Aston Villa Pepe Reina amethibitisha kuwa alikuwa na dalili za kuwa na virusi vya corona japo bado hajagundulika kama anavyo au la hiyo ameendelea kujitenga.
Pepe Reina ambaye aliwahi kucheza Liverpool, ameendelea kujitenga kama wachezaji wenzake wa Ligi Kuu walivyoshauriwa kufanya hii yote inatokana na hofu ya afya yake.
“Wiki iliyopita ilikuwa wiki yangu kukutana na mdudu (virusi) ilikuwa ni wiki ya tofauti na kuanza kuchukua tahadhari ya kuto athiri watu wanaoishi na mimi”>>> Reina VIA Radio Cope
England Ligi Kuu imesimamishwa hadi April 30 2020 kwa hofu ya virusi vya corona na inadhauriwa kuwa kila atakayehisi kuwa na dalili za virusi England ajitenge nyumbani kwake.

About the author

kidevu

Leave a Comment