Katibu mkuu wa Yanga SC David Luhago aeleza kuwa haoni tatizo kwa kinacholalamikiwa na baadhi ya wachezaji kuwa bonasi ya Tsh milioni 200 iliyotolewa na GSM kwa kuifunga Simba haipswi kulalamikiwa na wachezaji kwa sababu haipo kwenye mkataba.
Luhago ametoa ufafanuzi huo baada ya kuvuja kwa sauti za wachezaji wa Yanga David Molinga na Makame ambao hawakucheza mchezo na kupewa bonasi ya Tsh milioni 2.5 kwa kila mchezaji asiyecheza huku waliocheza wakipewa Tsh milioni 10 kila mmoja, Makame kwa mujibu wa voice note iliyovuja na kudaiwa kuwa yake hataki kuchukua pesa hizo kwa sababu anadaiwa kuona kama upendeleo.