HABARI

EPL haitorejea tena April 30 2020

Baada ya Ligi Kuu England wiki iliyopita kutangazwa kuwa imesogezwa mbele hadi April 30, leo imethibitika taarifa mpya kuwa Ligi hiyo haitorejea April 30.
Chama cha soka cha England (FA) kilitangaza kuwa Ligi zote za soka England ikiwemo EPL zinasimama hadi April 4, baadae wakasogeza hadi April 30 ila leo kwa mujibu wa mailsports.co.uk Ligi hairejei tena April 30.
Tarehe mpya wa mechi za Ligi Kuu England msimu wa 2019/2020 itatangazwa wiki ijayo, hii inatokana na hofu ya virusi vya corona kuzidi kutanda kila kona duniani.

About the author

kidevu

Leave a Comment