HABARI

Mwanamke amejiua akiwa karantini

Mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini amejitia kitanzi kwenye karantini ya Shule ya Ufundi nchini Kenya (KITI), iliyopo Mjini Nakuru, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya watu wanaoingia nchini humo kutoka Mataifa yaliyoripotiwa kuwa na ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Jeshi la Polisi nchini humo kupitia kwa Kamishna wa Nakuru George Natembeya, amethibitisha kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alijitoa uhai kwa kujinyonga na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hatua hiyo.
Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Afya kaunti ya Nakuru Dkt Kariuki Gichuki, amesema mwanamke huyo aliingia nchini Kenya Machi 25 mwaka huu na alitakiwa kusalia eneo hilo kwa siku 14, kabla ya kukutwa chumbani kwake akiwa amefariki.


About the author

kidevu

Leave a Comment