HABARI

Waziri Mkuu wa Uingereza akutwa na Virusi vya Corona

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amekutwa na coronavirus, baada ya kufanyiwa vipimo, imesema ofisi yake Downing Street.
“Nimekuwa na dalili ndogo za coronavirus, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi ,” Bwana Johnson amesema katika video aliyoituma kweinye ukurasa wake Twitter.
Johnson atajitenga binafsi – katika makao yake ya kikazi ya Downing Street, baada ya kupimwa na kupataikana na virusi hivyo na muhusumu wa huduma za afya nchini Uingereza katika ofisi yake al maarufu No 10.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa ataendelea kulingoza taifa kutoka nyumbani baada ya kupatikana na Covid-19.

About the author

kidevu

Leave a Comment