HABARI

Huu ndio mshahara atakaopokea Messi, Griezmann na Suarez wakikubali kukatwa 70% ya mshahara wao

Ni siku moja imepita toka iripotiwe kuwa wachezaji wa FC Barcelona wamegoma kukatwa asilimia 70 ya mishahara yao wakati huu wa virusi vya corona sababu ya cluba kukwepa hasara.
Leo umetoka mchanganuo wa baadhi ya wachezaji wa club hiyo endapo watakubaliana na suala la kukatwa mshahara kwa asilimia 70 wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.
Wachezaji kama Lionel Messi, Antoine Griezmann na Luis Suarez ndio wachezaji wanaolipwa pesa nyingi katika club hiyo, Messi analipwa pound 500,000 kwa wiki (Tsh bilioni 1.4) kama atakatwa asilimia 70 atalipwa pound 150000 (Tsh milioni 431).
Griezmann analipwa pound 294,000 (Tsh milioni 846) akikatwa 70% atalipwa pound 88200 (Tsh milioni 253), Luis Suarez pound 290,000 ( Tsh milioni 835) akikatwa 70% atalipwa pound 87,000 (Tsh milioni 250) malipo hayo ya mishahara ya wiki ni bila ya makato ya kodi.

About the author

kidevu

Leave a Comment