HABARI

Davido kathibitisha mpenzi wake kakutwa na Corona

Mwimbaji Star kutokea Nigeria Davido amethibitisha mpenzi wake Chioma kukutwa na virusi vya COVID-19 ( Corona Virus ) baada ya vipimo walivyomchukua March 25.
Davido ameeleza kuwa na mpenzi wake Pamoja na Watoto na watu wakaribu waliokuwa wamesafiri nao walichukua uamuzi wakujitenga baada ya kutoka safari nakurudia Nigeria ili kuangalia hali zao za kiafya kama zitakuwa hasijaathirika na ugonjwa huo.
Pamoja na Chioma kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona lakini Davido na wengine wote akiwemo mtoto wao hajapatwa na maambukizi hayo.
……>>> Washirika tumekutana nao kwa majaribio ya COVID-19 mnamo tarehe 25 Machi. Kwa bahati mbaya, matokeo ya mchumba wangu yalirudi yakiwa Positive wakati wengine wote 31 waliopimwa wamerudi kuwa Negative ikiwa ni pamoja na mtoto wetu.
”Bado tunaendelea vizuri kabisa na yeye bado bado hajaonyesha dalili zozote zile. Hivi sasa amewekwa Quarantine na pia nimeenda katika kujitenga kamili kwa siku 14.
Nataka kutumia fursa hii kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usio na mwisho na maombi mapema na kuwasihi kila mtu tafadhali kaa nyumbani kwani kutasaidia kudhibiti kuenea kwa virusi hivi! Pamoja tunaweza kuoambana na hii! — Davido

About the author

kidevu

Leave a Comment