HABARI

KLOPP:ITAKUWA NGUMU KUTETEA UBINGWA

 


 JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kwa mwendo ambao wanakwenda nao kwa sasa anaamini itakuwa ngumu kwao kutetea taji la Ligi Kuu England.

Liverpool inapita kwenye kipindi kigumu kwa sasa ndani ya uwanja kwa kuwa haipati matokeo chanya jambo linalompasua kichwa kocha huyo ambaye ni bingwa mtetezi.

Februari 22, ilikubali kichapo cha mabao 0-2 dhidi ya Everton ikiwa Uwanja wa Anfield na kuwafanya waporomoke kutoka nafasi ya nne mpaka ya sita.

Imecheza mechi 25 za Ligi Kuu England na imekusanya pointi 40 kibindoni kwa msimu wa 2020/21.

Klopp amesema:”Ligi ni ngumu na kila timu inahitaji kufanya vizuri hivyo ninaona kwamba kuna ugumu kwenye kutetea taji la ligi licha ya kwamba lolote linaweza kutokea,”.

Matokeo mabovu inayopata ni kutokana na kuwa na lundo la wachezaji wengi ambao wanasumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na beki kisiki Virgil Dijk, Fabinho.

About the author

kidevu

Leave a Comment