HABARI

MASAU BWIRE:PENALTI ILITUTOA MCHEZONI

 


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa mchezo wao wa jana walitolewa mapema kwenye ari ya ushindani baada ya wapinzani wao kupewa penalti yenye utata na mwamuzi wa kati ambaye alikuwa ni Martin Saanya.

Wakati Ruvu Shooting ikinyooshwa mabao 3-0 dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Karume, Mara, dakika ya 34 Saanya alitoa penalti kwa Biashara United.

Penalti hiyo iliyopachikwa kimiani na Christian Ziga dakika ya 36 ilileta utata kwa kuwa mpira ulionekana ukimgonga usoni nyota wa Ruvu Shooting, Casian Ponera.

Bwire amesema:”Hamna namna kwetu sisi kuonekana tumeshinda ama tumepoteza ila ukweli ni kwamba baada ya ile penalti naona kabisa ari ya wachezaji ilipungua.

“Kweli walitolewa mchezoni kwa ajili ya suala hilo hivyo ninawaomba mashabiki waamini kwamba timu yetu ipo imara na itaendelea kupambana kufikia malengo tuliyojiwekea,” .

About the author

kidevu

Leave a Comment