HABARI

TUCHEL ASHANGAZWA NA UWEZO WA GIROUD

 


KOCHA Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa nyota wake Olivier Giroud alimshangaza kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga bao aina ya acrobatic.

Bao hilo la Giroud  mwenye umri wa miaka 34 alipachika dakika ya 68 mbele ya Atletico Madrid ikiwa ni hatua ya 16 ndani ya uwanja wa taifa wa Arena linawapa nafasi ya kuweza kusonga mbele ikiwa watashinda ama sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa marudio.

Tuchel amesema kuwa hakutarajia kumuona nyota huyo akifanya hivyo licha ya kukukubali uwezo wake akiwa ndani ya uwanja kwa kuwa amekuwa akifanya vizuri kila anapopata nafasi.

Naye Giroud amesema kuwa hajui ni namna gani aliweza kufunga bao hilo la ushindi ila anachotambua yeye ni kwamba timu yake imeshinda jambo ambalo linampa furaha yeye pamoja na wachezaji kiujumla.

“Sijui kwangu ilikuaje na namna gani niliweza kufunga ndani ya uwanja ila kwa kuwa imeshatokea kwangu ni furaha na ni wakati wetu wa kupambana kwa ajili ya mechi zijazo na tuna amini tutafanya vizuri kwenye mchezo wetu wa marudio,”.

Tuchel amesema:-“Ukimuona ndani ya uwanja na namna ambavyo anajifunza kila siku lazima ushangae ila kwa namna ambavyo alifunga bao mimi mwenyewe nimeshangaa unaweza ukasema ni kijana mwenye miaka 24 kumbe ana miaka 34.

“Hatukuwa kwenye wakati mzuri kwa kuwa tumetengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia ila kwa kuwa tumeshinda itatuongezea nguvu kwenye mechi ya marudio,”.

About the author

kidevu

Leave a Comment